
Upinzani nchini Zimbabwe umemshutumu Rais wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa, kuwa ameonyesha upendeleo katika kuunda serikali yake, baada ya kumteua David Kudakwashe, ambaye ni mtoto wake, katika nafasi ya Naibu Waziri wa Fedha na Tongai Mnangagwa, ambaye ni mpwa wake katika nafasi ya Naibu Waziri wa Utalii.
.
Bado Hakujawa na majibu rasmi kutoka kwa chama tawala au Rais juu ya tuhuma hiyo, huku wafuasi wa Mnangagwa wakisema kuwa mtoto huyo wa Rais anastahili kushika nafasi hiyo.
