
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, amerejea Zanzibar mapema leo alfajiri akitokea China kwa Ziara ya siku ya siku nne aliyoianza tangu tarehe 27 June 2023.
Kwenye Uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Dk. Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi amepokewa na Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mheshimiwa Idrissa Kitwana Mustafa na viongozi wengine wa serikali na vikosi vya Ulinzi na Usalama.
Akiwa China Dr. Mwinyi alihudhuria Mkutano mkubwa wa tatu wa China na Afrika wa masuala ya ushirikiano wa kibiashara. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Rais wa Malawi Lazarus Chikwera na Makamu wa Rais wa China Mheshimiwa Han Zheng katika jiji la Changsha jimbo la Hunan.
Pia likiwa na mazungumzo na viongozi wa kampuni mbalimba za wawekezaji waliovutiwa kuja kuwekeza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
