Back to top

Rais Mwinyi ashuhudia utiaji saini miradi ya uwekezaji.

18 January 2022
Share

Rais wa Zanzibar Mh. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameshuhudia utiaji saini wa miradi mikubwa ya uwekezaji baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kampuni ya Eagle Hills Regional Properties ya Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE), ambao kwa upande wa Zanzibar ulifanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar(ZIPA) Shariff Ali Shariff na kwa upande wa Kampuni ya ‘Eagle Hills Regional Properties’ ulifanywa na Mohammed Ali Rashid Alabar.