Back to top

Rais Mwinyi azuia ujenzi wa hospitali mpya ya rufaa.

07 June 2021
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezuia ujenzi wa hospitali mpya ya rufaa na kumfuta mkandarsi wake na kuitaka Wizara ya Afya kuanza mchakato wake upya, gharama na mkandarasi wa ujenzi.

Uamuzi huo wa Rais Mwinyi umetolewa ndani ya Baraza la wawakilishi kwenye kikao cha bajeti na Waziri wa Afya, Mhe.Nassor Ahmed Mazrui ambaye amesema mpango wa awali ulikuwa na kasoro.

Mhe.Mazrui amesema wizara inajipanga upya na mchakto huo unaotaarjiwa kukamilika hivi karibuni na serikali itatoa uamuzi wa gharama na mkandarsi.

Katika hatua nyingne bajeti ya Waziri wa Fedha na Mipango, wajumbe waliipitisha bila ya kuwepo mvutano mkubwa.