Back to top

Rais Samia aitaka wizara ya Madini kusaidia wachimbaji wa dhahabu.

13 June 2021
Share

Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Madini kuwasaidia wachimbaji wadogo na wakubwa wa dhahabu ili wachimbe  dhahabu ya kutosha kukidhi mahitaji ya kiwanda cha kusafisha dhahabu Jijini Mwanza.

Pia ametaka kusiwe na urasimu wa kupindukia kwa watu kutoka nje ya nchi watakaoamua kuleta dhahabu kwenye kiwanda hicho, kwani kiwanda kina uwezo mkubwa wa kusafisha dhahabu na kinahitaji malighafi ya kutosha.

Kuhusu madini ya TANZANITE Rais Samia ameitaka Wizara ya Madini kuifanya TANZANITE kuwa na upekee kwa kuitambulisha kuwa ni madini yanayochimbwa Tanzania pekee.

Amesema Serikali haitaki kuona wawekezaji wameshikilia maeneo bila ya kuyafanyia kazi.

Rais Samia yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya siku tatu kukagua miradi mbalimbali na kuzungumza na wananchi.