
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan amekemea vikali vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya Maafisa Uhamiaji na hivyo, kusababisha zoezi la kukaribisha wawekezaji kutoka nje kuzorota.
Awali Mkuuwa Mkoa wa Tanga Bw.Omary Mgumba, amemuomba Rais Samia kufanya utaratibu wa kuzungumza na marais wa nchi za Ethiopia na Somalia kufuatia idadi kubwa ya wahamiaji kutoka nchini kwao ambao wamemaliza vifungo vyao, lakini bado hawajachukuliwa.
Rais Samia amehudhiria kufungwa kwa mafunzo ya wanajeshi wa Idara ya Uhamiaji.
Katika hafla hiyo vikosi vya Jeshi la Uhamiji vilivyotoa heshma kisha amiri jeshi mkuu a me toa vyeti kwa wanachuo waliofanya vyema katika mafunzo yao.
