Back to top

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MBOWE IKULU

04 March 2022
Share

Rais wa Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe.Freeman Aikaeli Mbowe, ambapo katika mazungumzo hayo Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki.

Hata hivyo Mhe.Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taifa la Tanzania ni kusimama katika haki.

Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na za kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipaswavyo.