
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kibali cha kuongeza posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma ambapo kwa kiwango cha juu, posho hiyo imepanda kutoka Tsh. 120,000 hadi Tsh. 250,000 na kiwango cha chini kutoka Tsh. 80,000 hadi Tsh. 100,000.
.
Aidha, Dkt.Ndumbaro akaongeza kuwa kiwango cha malipo ya kazi maalum (Extra Duty) kwa Watumishi kimeongezwa kwa ngazi zote ambapo kwa ngazi ya chini kimepanda kutoka Tsh. 15,000 hadi Tsh.30,000, ngazi ya kati kimepanda kutoka Tsh. 20,000 hadi Tsh.40,000 na ngazi ya juu kimeongezeka kutoka Tsh. 30,000 hadi Tsh. 60,000.
