Back to top

Rais Samia aonya Madiwani wanaotumia asilimia 10 kujiimarisha kisiasa.

08 June 2021
Share


Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ametoa onyo kwa baadhi ya madiwani katika halmashauri mbalimbali nchini wanaotumia asilimia 10 za halmashauri za makundi maalumu kujiimarisha katika siasa na wanaofanya ubadhirifu waache mara moja tabia hiyo na badala yake fedha hizo zitumike kuwasaidia wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Akizungumza na wanawake wa Jiji Dodoma kwa niaba ya wanawake nchi nzima Rais Samia ametumia fursa hiyo kuwakumbusha madiwani na makundi yanayopokea fedha hizo wakiwemo wanawake kuhakikisha wanazitumia kwa lengo lilokusudiwa na serikali.

Kuhusu sekta ya elimu Rais Samia amesema kunzia mwezi ujao, serikali inatarajia kujenga shule moja ya wasichana ya mchepuo wa Sayansi katika kila mkoa nchini.

Ameagiza kuwekwa utaratibu mzuri wa kulipa deni kwa mgonjwa aliyepo hospitali badala ya kuzuia maiti pale mgonjwa anapokuwa amefariki  dunia.