Back to top

RAIS SAMIA ARIDHIA VIJIJI 98 KUMEGEWA MAENEO YA HIFADHI TABORA

01 March 2024
Share


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, ameridhia Vijiji 98 kumegewa maeneo katika hifadhi mbalimbali mkoani Tabora, huku vijiji 2 vikiamriwa kuondoka kwa kuwa vimeingia ndani sana ya hifadhi.

Silaa ametoa kauli hiyo kwenye mkutano na wananchi wa Vijiji vya Ukumbi Kakoko na Usinge wilani Kaliua Mkoa wa Tabora , wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Kisekta wanaosimamia maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi ya Vijiji 975 nchini.