Back to top

RAIS SAMIA ARUDISHA MATUMAINI MBARALI

18 September 2023
Share

Makamu Mwenyekti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndg.Abdulrahaman Kinana, amewaambia wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amekubali ombi lao la kuendelea na shughuli za kilimo katika eneo lililozuiwa kupitia tangazo la Serikali la GN 28, kama ilivyokubaliwa mwaka jana.

Tangu kutolewa kwa katazo hilo, wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa mchakato wa kufikia maamuzi hayo haukuwa shirikishi na kuiomba serikali kuliondoa katazo hilo ambalo linaathiri ustawi wa maisha yao na kipato.

Kinana ameeleza hayo wakati akihitimisha kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya, zilizofanyika katika Kijiji cha Chimala, Makamu Mwenyekiti Kinana alisema mgombea Ubunge wa CCM Bahati Ndingo, Madiwani wa CCM, Viongozi wa CCM.