
Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema serikali anayoiongoza inathamini mchango wa vyombo vya habari katika kufichua maovu yanayofanyika sehemu mbalimbali nchini.
Kauli ya Rais Samia imetolewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya wahariri wa vyombo vya habari iliyoandaliwa na taasisi ya Uongozi Institute.
Amesema kupitia vyombo vya habari serikali imekuwa ikifanya Mambo mengi kwa jamii hivyo itaendelea kuiunga mkono sekta hiyo ili iweze kutimiza majukumu yake.
Aidha Waziri Nape amesema ataitisha kikao na wadau wa vyombo vya habari ili kujadili madhaifu ya sheria iliyopo Sasa ya sekta yahabari.
