Back to top

RAIS SAMIA AWAHAKIKISHIA WATOTO HAKI ZAO KULINDWA

16 June 2022
Share

Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewatakia maadhimisho mema ya Mtoto wa Afrika, Watoto hao na Jamii yote na kusema serikali itaendelea kuhakikisha haki za watoto zinalindwa.

Kupitia kwenye Ukurasa wake wa Twitter Mhe.Rais Samia ameandika ujumbe huo huku akisema "Tuendelee kutekeleza Ajenda ya 2040 inayotaka Bara la Afrika kuwa sehemu bora kwa mtoto kwa kupata ulinzi na huduma bora, ikiwemo elimu.


             TUJIKUMBUSHE

Leo tarehe 16 Juni 2022 Tanzania inaungana na Nchi zingine za Afrika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Chimbuko la Maadhimisho haya ni Azimio lililopitishwa na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mwaka 1990 kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini waliouawa tarehe 16 Juni, 1976 kutokana na ubaguzi wa rangi.

Watoto hao walikuwa wakidai haki zao za kutobaguliwa pamoja na haki nyingine za kibinadamu ikiwemo haki ya kupata elimu bora na hivyo kupinga mifumo ya elimu ya kibaguzi. Kufuatia tukio hili, OAU iliazimia kuwa tarehe 16 Juni ya kila mwaka iwe Siku ya Mtoto wa Afrika.

Bofya hapa.-ULIMWENGU LEO UNAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA