Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuungana katika Sensa ya Watu na Makazi na kusema kuwa sensa ijayo itakuwa na mabadiliko tofauti na za miaka iliyopita.
.
Amesema kutakuwa na ongezeko la dodoso la idadi ya majengo nchi nzima hali itakayosaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi.
.
Rais Samia ameyasema hayo Jijini Dodoma kwenye uzinduzi wa mkakati wa uelimishaji na ushirikishwaji wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka ujao.
.
Ameitaka kamati ya taifa ya sensa kuwekeza katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa.
.
Kwa upande wake Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara, Mhe.Anne Makinda amesema sensa hiyo ni shirikishi na inaanzia ngazi ya kitongoji na kuwataka Watanzania kuona fahari kuhesabiwa.