
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrhaman Kinana, amezungumzia mjadala wa uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam, ambapo amewataka watanzania kuwa na imani na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoingoza, kwani hawezi kuuza Bandari hiyo.
.
Kinana ameyasema hayo, wakati akizungumza na wananchi mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo, Musoma Mjini, huku akibainisha kuwa uwekezaji huo utasaidia kuongeza ufanisi wa bandari na kukuza uchumi wa Tanzania.
