
Mh. Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake ina mipango ya kuanzisha kiwanda cha kuzalisha chanjo za COVID-19 na maradhi mengine ndani ya nchi.
.
Rais Samia ameyasema hayo akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya (European Council) Mh. Charles Michel, wakati wa ziara yake nchini Ubelgiji, ambapo alibainisha kuwa bajeti ya serikali ya Tanzania kununua chanjo inakadiriwa kuongezeka kutoka shilingi bilioni 26.1 mwaka 2020 hadi bilioni 216 ifikapo mwaka 2030, ambayo ni sababu muhimu ya kujenga kiwanda hicho.
