Back to top

RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA MAOFISA DAR ES SALAAM

02 September 2023
Share

Jeshi la Polisi Tanzania, linatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Maofisa wakuu waandamizi, kutoka Makao Makuu, mikoa na vikosi kuanzia Septemba 04, 20223 Jijini Dae es Salaam, kutathmini ya utendaji kazi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Msemaji wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, David Misime amesema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Amesema katika mkutano huo mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalam kutoka vyuo vya hapa nchini na wataalam wa kada mbalimbali.

Amesema Maafisa washiriki watapata fursa ya kufanya tathmini ya majukum ya Jeshi la Polisi na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa mwaka 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.