
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na Rais Yoweri Museveni wa Uganda pamoja na Rais wa Kenya, William Ruto, katika Ikulu ndogo iliyopo Tunguu kisiwani Zanzibar.
.
Katika mazungumzo yao Marais hao watatu, wamezungumzia masuala ya mtangamano wa Afrika Mashariki hususan umuhimu wa kuharakisha zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi Juu ya muundo na maeneo ya kuangaliwa katika Rasimu ya Katiba ya Fungamano la kisiasa la Afrika Mashariki.
.
Zoezi hilo limeshafanyika katika nchi za Burundi, Uganda na Kenya na linatekelezwa na Timu ya Wataalamu inayoundwa na Wajumbe watatu kutoka kila nchi Mwanachama.
