Back to top

Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ziara ya siku 3 mkoani Mwanza.

07 June 2021
Share

Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani Mwanza ukiwemo wa ujenzi wa daraja la JPM, kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa SGR eneo la fela na kuzindua mtambo wa kuchenjua dhahabu pamoja na kuzungumza na wananchi kuanzia Juni 13 hadi 15.

Taarifa ya ziara ya Rais Samia, imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila ambapo ameeleza kuwa Mhe.Rais mbali na kukagua miradi hiyo, kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa reli ya kisasa SGR pia atazungumza na vijana kuhusu fursa za ajira na uchumi.