
Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, amezindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara.
Rais Samia amesema kuwa kukamilika kwa Hospitali hiyo, ambayo ina watalaam, vifaa na vifaatiba vya kisasa itasaidia watu wa Kanda ya Kusini inayojumuisha Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kupata uhakika wa huduma za matibabu ya kibingwa karibu na maeneo yao.
Rais Samia amesema kuwa kazi ya watumishi wa afya ni kuokoa maisha ya watu hivyo watumishi hao wajitumie kufanya kazi kwa kuwa Serikali imewekeza kwenye miundombinu, vifaa na dawa na wao watimize wajibu wao.
Tunahitaji matunzo ya jengo hili, vifaa na huduma kwa wananchi kwa lugha nzuri, kila mtu amepangiwa jukumu lake na Mwenyezi Mungu, tumridhishe Mungu kwa huduma tunazozitoa, nawatakia kila la kheri” amesema Rais Samia huku akiongezea kuwa changamoto zilizopo za watumishi zitaendelea kufanyiwa kazi kwa haraka.
