Back to top

RAIS TINUBU AFUTA KAZI WAKUU WA USALAMA, NIGERIA

20 June 2023
Share

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu, amewafuta kazi wakuu wa usalama wa nchi hiyo na wakuu wa polisi, akiwemo Mkuu wa ulinzi, mkuu wa jeshi, jeshi la wanamaji na jeshi la wanahewa wote walistaafishwa na nafasi zao kuchukuliwa na maafisa wapya.

Taarifa rasmi zinaeleza kuwa Bw.Tinubu ameidhinisha kustaafu mara moja kwa wakuu wote wa huduma na Inspekta Jenerali wa polisi, washauri, mdhibiti mkuu wa forodha kuacha majukumu na mabadiliko hayo kutekelezwa mara moja.

Bw.Tinubu pia amevunja bodi za taasisi zote za serikali, lakini bila kujumuisha zingine zikiwemo Baraza la Mahakama, baraza la uchaguzi na tume ya huduma ya polisi.

Mabadiliko hayo ya usalama yanajiri wiki mbili baada ya Rais kukutana na wakuu wa usalama na kuwaamuru kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na changamoto za ugaidi, uasi, ujambazi, wizi wa mafuta na uharamia.

Nigeria imekuwa ikikabiliwa na wimbi la mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na makundi ya kijihadi na magenge mengine ya wahalifu, wakiwemo majambazi ambao hujihusisha zaidi na utekaji nyara ili kujipatia fidia.