Back to top

Ramaphosa ataka uwakilishi wa Afrika katika Umoja wa Mataifa.

23 September 2020
Share


Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais wa Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametaka idadi ya nchi za Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iongezwe.

Akihutubia mkutano wa sabini na tano wa Umoja wa Mataifa kwa njia ya video amesema mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja huo yatasaidia katika kusuluhisha migogoro duniani.

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Afrika amesema muundo wa sasa wa baraza hilo hauendani na hali ya sasa na katika Maadhimisho ya miaka sabini na mitano ya kuanzishwa kwa umoja huo, ametaka wawakilishi zaidi wa nchi za Afrika katika Baraza la Usalama.

Kwa sasa Afrika Kusini ni mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.