Back to top

Ramon Abbas akiri kosa la utakatishaji fedha Mahakamani.

30 July 2021
Share


Mtu mashuhuri katika mtandao wa Instagram raia wa Nigeria Ramon Abbas maarufu kwa jina la 'Hushpuppi' amekiri kosa katika mahakama nchini Marekani la utakatishaji fedha.

Alikamatwa, sambamba na washukiwa wengine, huko Dubai mwezi Juni mwaka jana kwa shutuma za ulaghai wa kiasi cha dola milioni 1.1 za Marekani zinazohusishwa na ufadhili wa shule.

Hushpuppi alirejeshwa Marekani ili kuyakabili mashtaka dhidi yake.

Nyaraka zake za kujibu mashtaka zimeonesha kuwa alikiri kuhusika katika sakata ya ufadhili wa shule na vitendo vingine vya ulaghai ikiwemo kinachojulikana kama barua pepe za kibiashara na kuwahadaa watu kupitia mitego iliyohusisha dola milioni 24 taarifa ya Ofisi ya mwendesha mashtaka marekani imesema.

Nyaraka zake za kujibu mashtaka zinaonesha kwamba alikiri kuhusika katika mpango wa fedha za shule na kama shughuli zingine za ulaghai, pamoja na ile inayojulikana kama mipango ya biashara ya barua pepe, ambayo ilifikia dola milioni 24.