
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. John Mongella, ambaye ni mwenyekiti wa Usalama Mkoani humo, amesema kuwa thathimini iliyofanyika imebaini kuwa wageni wengi, wanaridhika na Usalama wa Mkoa huo ambao no kitovu cha utalii hapa nchini.
Kauli hiyo ametoa katika hafla ya Polisi day, ambapo amewapongeza askari waliofanya kazi vizuri zaidi na kutoa huduma bora Kwa wananchi wanao litegemea Jeshi hilo.
Ameongeza kuwa katika Mikoa iliyopo hapa nchini Mkoa wa Arusha, umeonyesha hali ya usalama kuhimarika Mkoani humo, huku akiwataka askari kuendelea na utaratibu wa kupongezana kutokana na Juhudi kubwa, ambazo wanafanya za kuimarisha ulinzi kitendo kilichopelekea Mkoa huo kuwa shwari.
Mongella amebainisha kuwa wageni wa ndani na wale wanaotoka mataifa ya Afrika na Ulaya, wameonyesha kuridhishwa na Usalama na utulivu wa jiji hilo na Mkoa wa Arusha Kwa ujumla.
Pia amewataka askari wao kujikita katika kutoa elimu katika jamii, sambamba na dhana ya Polisi jamii na namna bora ya ushirikishwaji jamii Ili kubaini na kutanzua uhalifu katika Mkoa huo ambao no kitovu cha utalii hapa nchini.
Sambamba na hilo amewataka askari hao kufuataratibu za Jeshi hilo huku akiwataka wale wenye Mapungu yanayolichafua Jeshi kujirekebisha ili kuishi katika misingi ya Jeshi hilo.
