Back to top

RC Mtwara aagiza kusimamishwa kazi Kaimu Meneja chama cha ushirika.

10 June 2021
Share

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Marco Gaguti ameiagiza bodi ya chama kikuu cha ushirika cha masasi Mtwara Mamcu kumsimamisha kazi Kaimu meneja  wa chama hicho Potency Lwiza na nafasi yake kujazwa ndani ya saa 24  ili kupisha uchunguzi wa tuhuma  zinazomkabili zikiwemo  za matumizi mabaya ya ofisi.

Mkuu wa mkoa amesema hayo katika kikao na wajumbe wa bodi ya chama hicho pamoja na watendaji wa chama hicho na kuamuru bodi ya chama hicho kumsimamisha kazi mara moja.

Amesema pamoja na kusimamishwa kazi ameitaka bodi hiyo kuhakikisha nafasi hiyo anatafutwa mtu mwingine ili kazi ziendelee wakati uchunguzi wa meneja aliyesimamishwa kazi ukiendelea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho Siraji Mtenguka amesema wamepokea maagizo ya mkuu wa mkoa na wanayatekeleza ndani ya saa ishirini na nne.

Hata hivyo mwenyekiti huyo amesema meneja huyo amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya uendeshaji wa ofisi.