
Kifaa cha upasuaji chenye ukubwa wa sahani ya chakula, kimekutwa ndani ya fumbatio la mwanamke miezi 18, baada ya kujifungua mtoto wake kwa njia ya upasuaji (cesarean section), kwa mujibu wa ripoti ya Kamishna wa Afya na Ulemavu wa New Zealand.
Kifaa hicho kiitwacho Retractor Alexis, ambacho kinaweza kupima sentimeta 17 (inchi 6) kwa kipenyo, kiliachwa ndani ya mwili wa mama huyo wakati wa upasuaji katika Hospitali ya Jiji la Auckland mnamo 2020.
Mwanamke huyo alipata maumivu ya muda mrefu kwa miezi kadhaa na alienda kuchunguzwa mara kadhaa ili kujua ni nini kilikuwa kiki msumbua, X-ray haikuonyesha dalili yoyote ya kifaa hicho, lakini kifaa kiligunduliwa kwenye CT scan ya tumbo na kuondolewa mara moja mnamo 2021.
Taarifa hiyo imewekwa wazi Septemba 04,2023 katika maamuzi ya kesi mbele ya Kamishna wa Afya na Ulemavu wa New Zealand, Morag McDowell ambapo ameitaka Bodi ya Afya ya Wilaya ya Auckland iombe msamaha kwa maandishi kwa mwanamke huyo na kurekebisha sera zake.
Kesi hiyo pia imewasilishwa kwa mkurugenzi wa kesi, afisa ambaye ataamua ikiwa hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa.
Dkt Mike Shepherd, Mkurugenzi wa operesheni wa kikundi cha Te Whatu Ora Health New Zealand aliomba radhi kwa kosa hilo kwa maandishi.
"Tungependa kuwahakikishia umma kuwa matukio kama haya ni nadra sana, na tunasalia na uhakika katika ubora wa huduma zetu za upasuaji na uzazi."Dk.Mike.
