Back to top

RIDHIWANI AWATAKA WENYEVITI MABARAZA YA ARDHI KUJIEPUSHA NA RUSHWA

06 April 2022
Share

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Ridhiwani Kikwete amewataka Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya nchini kuwa waadilifu sambamba na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kutenda haki wakati wa kutoa maamuzi ya mashauri yanayohusu migogoro ya ardhi.

Ridhiwani amezitaka Mamlaka za Nidhamu kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wasiotimiza wajibu wao au wanaoidhalilisha serikali kwa kuendesha vitendo vya rushwa.

Ameongeza kuwa Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na nyumba ya wilaya nchini pamoja na Wasajili Wasaidizi wanakutana mkoani Tanga kwenye kikao kazi na mafunzo cha siku nne kujadiliana namna bora ya kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma bora kwa wananchi kuhusiana mashauri ya ardhi.