
Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amemuhamishia Makao Makuu ya Polisi Dodoma aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa ili kupisha uchunguzi wa tukio la Machi 26, 2022 ambapo amedaiwa kutoa maneno yaliyoonyesha kuwepo kwa ukiukwaji wa nidhamu kulingana na miongozo ya Jeshi la Polisi.
.
ACP Wankyo Nyigesa alirekodiwa katika sherehe ya kumuaga iliyofanyika mkoani Pwani, akimuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumpa Ukuu wa Jeshi la Polisi Nchini huku akiahidi kufanya makubwa katika nafasi hiyo.

