Back to top

Rufaa zingine 60 zatolewa uamuzi.

12 September 2020
Share

Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa 60 kati ya hizo rufaa 2 ni za Wagombea Ubunge na 58 ni za Wagombea Udiwani na taarifa ya mamuzi hayo imetolewa Septemba 11, 2020 na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Mahera. 

Matokeo ya rufaa za wagombea Ubunge ni kama ifuatavyo: 

i. Imekubali rufaa moja na kumrejesha mgombea katika orodha ya wagombea na rufaa hiyo ni kutoka kwenye Jimbo la Iramba Magharibi.
 
ii. Imekataa rufaa moja ya mgombea ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na rufaa hiyo ni kutoka kwenye Jimbo la Iramba Magharibi. 


Aidha, Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 58 za Madiwani, kama ifuatavyo: 

i. Imekubali rufaa 34 na kuwarejesha wagombea katika orodha ya wagombea Udiwani. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Kahororo (Bukoba), Ishozi (Nkenge),Chongoleani (Tanga Jiji), Kirare (Tanga Jiji), Mwamanga (Magu), Ngʻhaya (Magu), Riroda (Babati Vijini), Maswa Magharibi (Maswa), Kirumba (Ilemela), Bonga (Babati Vijini), Kamagambo (Karagwe), Namelock (Kiteto), Masewa (Bariadi), Bweranyange (Karagwe), Kituntu (Karagwe), Kamagambo (Karagwe), Msowero (Kilosa), Lubugu (Magu), Lingeta (Meatu), Ifakara (Kilombero), Kiloli (Sikonge), Mkoma (Rorya), Nyamhongolo (Ilemela), Sikonge (Sikonge), Tanganyika (Muheza), Uhenga (Wanging'ombe), Babati (Babati), Vwawa (Mbozi), Lukanga (Mkuranga), Langai (Simanjiro), Lutale (Magu), Majohe (Ilala), Namabengo (Namtumbo) na Viwanja Sitini (Kilombero). 

ii. Imekataa rufaa 23 za wagombea ambao hawakuteuliwa. Rufaa hizo  ni kutoka kwenye Kata za Ilemela (Ilemela), Kayenze (Mwanza Jiji), Kiarare (Tanga Jiji), Mabawa (Tanga Jiji), Ilemela (Ilemela), Kadoto (Maswa Magharibi), Iyela (Mbeya Jiji), Kirua Vunjo Magharibi (Vunjo), Mji Mpya (Morogoro Mjini), Pugu (Ukonga), Tembela (Mbeya Mji), Vikumburu (Kisarawe), Mecco (Ilemela), Kibara (Mwibara), Kiloleli (Sikonge), Changarawe (Mafinga Mji), Igawilo (Mbeya Mjini), Msonga (Mkuranga), Uru Kaskazini (Moshi Vijini), Kivukoni (Ilala), Maanga (Mbeya Mjini), Nsalaga (Mbeya Mjini) na Jangwani (Ilala).
 
iii. Imekataa rufaa 1 ya kupinga walioteuliwa. Rufaa hiyo ni kutoka kwenye Kata ya Arri (Babati Vijijini). 

Idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea Ubunge zilizofanyiwa uamuzi na Tume kufikia 113 na za wagombea Udiwani 103. Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku. Wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume.