Back to top

RUTO AMUONYA ODINGA DHIDI YA MAANDAMANO

16 March 2023
Share

Rais wa Kenya, William Ruto, amemuonya kiongozi mkuu wa upinzani, Raila Odinga, dhidi maandamano kwa Umma yaliyopangwa na Muungano wa upinzani wa Azimio, yatakayofanyika 20 Machi, 2023.

Rais Ruto amesema hatamruhusu, Odinga kufanya maandamano yatakayohatarisha maisha ya Wakenya, uharibifu wa mali au kulemaza shughuli za biashara nchini humo, nakubainisha kuwa Kenya ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria.