Back to top

Rwanda yaripoti idadi kubwa ya waliopona corona.

18 May 2020
Share

Wagonjwa 19 wamepona ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona nchini Rwanda huku watatu wakitajwa kuambukizwa virusi hivyo baada ya sampuli 1135 za vipimo kuchukuliwa ndani ya masaa 24 yaliyopita.

Hii ndiyo idadi kubwa ya watu waliopona virusi vya corona kuwahi kutangazwa tangu ugonjwa huo uripotiwe nchini humu tarehe 14 machi mwaka huu.

Rwanda imeripoti jumla ya watu waliopona virusi hivyo 197 na kesi 292 ikiwa ni pamoja na ongezeko la wagonjwa 3 waliopatikana baada ya sampuli 1135 za vipimo vilivyochukuliwa masaa 24 yaliyopita.