Back to top

SABA MATATANI UDANGANYIFU MTIHANI DARASA LA 7

22 September 2023
Share

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limewahoji watu 7, kwa tuhuma za kufanya udanganyifu wa mitihani ya darasa la saba, kwa kuwachukua wananfunzi wa sekondari na kuwafanyisha mitihani hiyo kwa niaba ya wanafunzi wa darasa la saba.
.
Tukio hilo lilitokea Septemba 13, 2023, katika shule ya msingi Igulumuki, Kata ya Igulumuki, wilayani Sengerema, wakati kamati ya mitihani ya Wilaya hiyo ilipotembelea shule hiyo kwa ajili ya ukaguzi, ndipo ilipobaini udanganyifu huo, ambapo mkondo namba 2 na 3, kulikuwa kumeingizwa wanafunzi wa Sekondari watatu.