Back to top

Safari ya Mwisho ya mpiga picha wa ITV Evarist Otaru yahitimishwa Mbez

21 March 2018
Share

Siku ya tarehe 20 March 2017 Vilio simanzi na Majonzi vilitawala katika maziko ya aliyekuwa mpigapicha Mwandamizi wa kituo cha utangazaji cha ITV/REDIO ONE EVAREST OTARU aliyefariki dunia March 16 Mwaka huu katika hospital ya taifa Muhimbili kwa Saratani ya Koo wakati waombolezaji wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mpiga picha huyo.


Wakati wa kutoa heshima za mwisho ikiwa ni muda mfupi baada ya paroko wa parokia hiyo Padre Sunil Kishor kuwataka waombolezaji kujiandaa na kifo.

Akisoma wasifu wa marehemu mtoto wa marehemu  humphery evarest amesema baba yao alikuwa  mwenye upendo  na msimamizi wa haki na amezaliwa mkoa wa kilimanjaro.

Akitoa shukrani kwa waombolezaji mdogo wa marehemu Bw. Deo Evarest amesema marehe ndio alikuwa kiongozo wao  kwania baba yao alishariki huku Bw.Deogratius Rweyunga akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/REDIO ONE amesema kampuni imempoteza mfanyakazi aliyejituma.

Marehemu Otaru ameacha mke na watoto watatu pamoja na mjuu mmoja na kabla ya kufikwa na Mauti.

Marehemu Otaru amefariki bado akiwa ni mfanyakazi wa kituo cha ITV/REDIO ONE kama mpiga picha kazi aliyotumia hadi kufikwa na umauti wake.