
Tetesi za Soka Ulaya , Manchester United na Manchester City watamenyana kuwania saini ya winga wa Brighton Mjapani Kaoru Mitoma mwenye umri wa miaka 26 mwezi Januari. (Fichajes - kwa Kihispania)
Lakini klabu zote mbili za Manchester zinaweza kukosa nafasi huku Mitoma akitarajiwa kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na Seagulls. (London World)
Nafasi ya Erik ten Hag kama meneja wa Manchester United iko salama kwa siku zijazo, licha ya msimu mbaya wa klabu hiyo. (Guardian)
