Back to top

SAKATA LA KINA MDEE NA WENZAKE, MAHAKAMA KUTOA UAMUZI.

16 May 2022
Share

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Tulia Ackson amesema hatma ya ubunge wa wabunge 19 waliovuliwa uanachama na chama chao kupitia Maamuzi ya Baraza Kuu la CHADEMA kubariki uamuzi wa kamati kuu ya chama hicho utasubiri maamuzi ya Mahakama.

Akitoa taarifa Bungeni kuhusu suala hilo Spika amesema wabunge hao wamepinga suala hilo Mahakamani.

Amesema kwa kuheshimu mamlaka za muhimili mwingine bunge litasubiri maamuzi ya mahakama ambayo kwa mujibu wa katiba ndio mamlaka ya mwisho ya uamuzi kuhusu haki hapa nchini.

Mh.Spika pia amekiri kupokea barua ya CHADEMA kuhusu maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na kusisitiza kuwa msemaji mkuu wa wabunge hao  kwa swali lolote ni Spika mwenyewe.