Back to top

Samia amteua Rogatus Hussein mtendaji mkuu TANROADS, Mgaya TAFICO.

30 July 2021
Share

Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bwana Rogatus Hussein Mativila kuwa Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Bwana Mativila anachukua nafasi ya Marehemu Mhandisi Patrick Mfugale ambaye alifariki dunia tarehe 29 Juni, 2021, kabla ya uteuzi huo Bwana Mativila alikuwa Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).

Pia amemteua Prof. Yunus Daud Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).

Prof.Mgaya ni Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, mbali na kuteuliwa kuwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la uvuvi Tanzania (TAFICO).