Back to top

SAMIA ATAKOPA KWA MAENDELEO YA WATANZANIA.

05 January 2022
Share


Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza dhamira yake ya kuendelea kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.

Amesisitiza dhamira hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea taarifa ya matumizi ya fedha za Uvico 19 ambazo ni mkopo wa shilingi Trilioni 1.3 kutoka Benki ya Dunia.

Amewataka viongozi wa serikali wakasimamie vivuri matumizi ya fedha hizo ili zikalete matarajio yaliyokusudiwa.

Aidha, ameelezea kuridhishwa kwake na matumizi ya fedha hizo katika miradi inayotekelezwa katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya na miundombinu ya barabara.

Rais Samia ameelezea kushangazwa kwake na watu wanaobeza juhudi zake za kutafuta fedha kwa njia ya mikopo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na kusisitiza kuwa serikali anayoiongoza siyo ya kwanza kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, kwani zilizotangulia pia zilifanya hivyo.

Amesema ataendeleaa kutafuta mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kama sehemu ya utekelezaji wa kiapo  chake alipokabidhiwa dhamana ya kuliongoza taifa.