
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan amempa miezi 6, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kuhakikisha hakuna mgao wa umeme.
.
Rais Samia ameyasema hayo kwenye hafla ya uapisho wa viongozi mbalimbali wateule, ambapo alibainisha kuwa kuna changamoto ya upungufu wa umeme ambayo imetokana na mitambo ya kuzalishia umeme kufanyiwa matengenezo kwa pamoja, baada ya kukaa muda mrefu bila kufanyiwa matengenezo.
.
"Nyamo-Hanga unakwenda TANESCO nikijua kwamba wewe si mgeni wa TANESCO unaijua vizuri...kwa hiyo utakwenda kuongeza pale Maharage alipofikia, tuna crisis...ile ni yetu kama Taifa, si ya mtu, maana mtu anaweza kusema sababu ya kukatikatika umeme kaondoshwa, hapana si kozi yake, ni kozi yetu kwa pamoja kwamba mitambo ile kwa muda mrefu haikufanyiwa service, sasa tunakwenda kuifanyia service kwa pamoja na unapofanya service kuna mingine ibidi izime, mingine iwake, kwa hiyo kuna upungufu wa umeme...kwa hiyo nenda kaanzie pale maharage alipoishia, najua utaweza nakupa miezi sita" Alisema Rais Samia Suluhu Hassan
