Back to top

SANAMU LA ASKARI LIPO, MRADI WA BRT HAUTOLIGUSA

12 June 2024
Share

Baada ya sintofahamu juu sanamu la askari lililopo Makutano ya barabara ya Samora na Azikiwe Dar es Salaam kwamba litaondolewa kutokana na ujenzi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) ni kwamba sanamu hilo halitoguswa wala kuondolewa eneo hilo kama taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni kwamba litaondolewa.

ITV Digital imefika eneo hilo na kukuta sanamu hilo likiwa lipo na shughuli nyingine zikiendelea katika eneo hilo.

Ni kwamba Mnara Askari ulijengwa mwaka 1927 na Utawala Mwingereza kwa kutambua mchango wa askari wa Kiafrika katika vita Kuu ya kwanza ya Dunia mwaka 1914 - 1918.

Mnara huu unahifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mambo ya Kale, Sura 333 na sheria ya Makumbusho ya Taifa sura 281, na ulitangazwa kuwa urithi wa taifa kupitia tangazo la serikali No.498 la mwaka 1995.