
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa ameshika utepe pamoja na viongozi mbalimbali, wakati Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, akikata utepe huo kuashiria uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia leo Februari 18, 2024.
.
Sanamu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere imewekwa kwenye makao makuu hayo, kwa ajili ya kutambua mchango wake katika masuala ya ukombozi Barani Afrika.

