Back to top

Saratani: wagonjwa wapya 42,060 kila mwaka

10 April 2022
Share

Waziri wa Afya Mhe.Ummy amesema Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa saratani 42,060 kila mwaka ikiwa ni sawa na wagonjwa 76 katika kila watu 100,000 huku vifo vikiwa ni 29,000 kila mwaka sawa na 68% huku wagonjwa wengi wakigundulika kuwa na ugonjwa huo ukiwa umefika katika hatua ya tatu au ya nne ambayo ni ngumu kutibika.
.
Mhe.Ummy ameyasema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kituo cha cha kisasa cha matibabu ya saratani ambacho kinatekelezwa kwa ubia kati ya Serikali pamoja na Taasisi ya Agha Khan, Jijini Dar Es Salaam.