Back to top

SCHOOL BUS ZIWE NA WALEZI WAWILI, WAKIKE NA WAKIUME

23 May 2024
Share

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa, amesema kuna kanuni ambazo wameziweka kwa ajili ya mabasi ya shule ambapo mojawapo ni pamoja na magari hayo kuwa na walezi wawili, mwanamke na mwanaume, kwa magari ambayo yanabeba wanafunzi wa kike na wa kiume, ili inapotokea dharura, mfano kwa mtoto wakike iweze kushughulikiwa na mlezi wa kike.
.
Mhe.Majaliwa ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe.Nancy Hassan Harusi, aliyeuliza, Je, serikali haioni haja ya kutunga sheria ya kulinda mabasi yote yanayosafirisha wanafunzi nchini? ambapo pia amesisitiza kuwa magari hayo pia yanapowapeleka watoto hao likizo, walezi hao wanatakiwa kuhakikisha wanawafikisha watoto hao mpaka kwa wazazi wao.
.
Amesema kanuni zingine zilizowekwa kwa ajili ya magari hayo ni pamoja na magari hayo kupakwa rangi ya njano, ili popote linapopita lijulikane kuwa hili ni basi la shule na liwe na maandishi makubwa mbele kuonyesha hili ni basi la wanafunzi (School Bus).