Wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi nchini ambazo ni ujenzi, wafanyabiashara ndogo ndogo na sekta ya usafiri wametakiwa kujiunga na mifuko ya hifadhi jamii ili kujihakikishia ulinzi wa huduma mbalimbali pindi wanapopoteza kazi huku serikali ikiombwa kuongeza juhudu ya kuelimisha kundi hilo.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam kufuatia utafiti uliofanywa na vyuo vitatu, chuo cha Mzumbe, chuo cha Nairobi chuo na chuo cha Rocksile kilichopo Denmark, ambapo Profesa Godbertha Kinyondo amesema utafiti huu utasaidia watunga sera na serikali kutafuta namna nzuri ya kutatua changamoto za wafanyakazi wasio katika sekta rasmi na zisizo ratibiwa.
Aidha Profesa Winnie Mitura alisema kukosekana kwa huduma muhimu za ulinzi wa jamii sio changamoto ya Tanzania pekee bali nchi nyingi za Afrika.
Kwa upande wake afisa mkuu mwandamizi kitengo cha hiari NSSF Bwana Abbas Cothema alisema tokea mwaka 2012 kuna ongezeko kubwa la usajili wa hiari kwa sekta zisizo rasmi ambapo walianza na watu elfu 30 mpaka sasa ni zaidi ya laki moja na 25 waliojisajili katika mifuko ya jamii na pia bado zaidi ya watu mil 21 hawajajisajili.