Back to top

Sekta ya madini yachangia kuongeza mapato ya taifa.

22 February 2020
Share

Waziri wa madini Mhe.Dotto Biteko amesema sekta ya madini imechangia ongezeko la mapato serikalini katika ukusanyaji wa kodi hapa nchini baada ya mapato kuongezeka kutoka shilingi bilioni 196 mpaka 335 kwa mwaka.

Waziri Biteko ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini Tanzania na kusema mafanikio hayo yamefikiwa baada ya wachimbaji na wawekezaji katika sekta hiyo kutambua umuhimu wa kuuza madini katika masoko maalumu yaliyoanzishwa hapa nchini na kuondoa vitendo vya urasimu katika soko la madini huku waziri wa nchi anayeshughulikia maendeleo ya madini nchini Uganda Mhe.Sara Upendi akisisitiza umuhimu wa kuwa na sheria kali za kulinda rasilimali madini barani Afrika.

Wakiwasilisha maoni yao kwa serikali baadhi ya wawekezaji katika sekta ya madini hapa nchini wamesema mazingira ya kununua madini kwa sasa yamekuwa rafiki kutokana na utekelezaji wa sheria mpya pamoja na uwepo wa mikutano hiyo, unawapa fursa kutoa maoni ya changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wao baadhi ya wachimbaji wadogo pamoja na idara mbalimbali zinasimamia sekta ya madini wakaelezea fursa za mikutano hii ya kimataifa katika kutangaza rasilimali mali madini yanayopatikana hapa nchini.