
Waandamanaji nchini Senegal wameingia barabarani, kupinga uamuzi wa Rais Macky Sall wa kuahirisha kwa muda usiojulikana, uchaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 25 mwaka huu.
Miongoni mwa waliokamatwa wakati maandamano hayo ni Waziri Mkuu wa zamani Aminata Touré na Anta Babacar Ngom, ambaye ni mmoja wa wagombea urais katika uchaguzi huo.
Wakati wabunge wa shirikisho wakijiandaa kujadili mswada utakaopitisha uamuzi huo wa rais Sall, viongozi wa upinzani walitoa wito kwa wananchi kutetea demokrasia.
Serikali ilisitisha matangazo ya televisheni ya kibinafsi ya Walf iliyokuwa ikipeperusha maandamano hayo moja kwa moja.
