Back to top

SENETA JELA MAISHA KWA MAUAJI YA RAIS

20 December 2023
Share

Mahakama ya Marekani, imemhukumu seneta wa zamani wa Haiti kifungo cha maisha jela, kwa kupanga njama ya mauaji ya Rais wa Haiti Jovenel Moise mwaka wa 2021.

Joseph Joel John, alihukumiwa na mahakama ya Shirikisho ya Miami, baada ya kukiri makosa matatu mwezi Oktoba, likiwemo la kula njama ya kuua na kumteka nyara mtu nje ya Marekani, na kutoa msaada wa mali na rasilimali kutekeleza njama ya kumuua Moise.

 

Moise aliuawa wakati wa shambulizi, kwenye makazi yake binafsi, katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince mnamo Julai 7, 2021. 

Mke wa rais wa Haiti, Martine Moise, pia alipigwa risasi lakini baadaye akapona.