Back to top

Serikali imetenga fedha za matengenezo ya barabara ya Kimara Bonyokwa.

04 May 2018
Share


Serikali imetenga fedha za matengenezo ya barabara ya kutoka Kimara mwisho hadi Bonyoka Segerea ili kuhakikisha inapitikana vizuri wakati wote.

Akijibu swali la Mbunge Ubungo Mhe said Kubenea ni lini serikali itaanza kujenga barabara kwa lami ambavyo miaka mitano iliyopita na serikali ya wamu ya nne kutoka Kimara mwisho kupitia Mvula hadi Bonyokwa Segerea  yenye urefu wa kilimita 4.7.

Naibu Waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa amesema utekelezaji wa  barabara ya Kimara mwisho kupitia Mavulunza hadi Bonyokwa Segerea kuunganisha barabara ya Nyerere yenye urefu wa kilimita 8 unategemea kuanza baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa mpango wa sasa wa ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano zinazoendelea.

Amesema utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano jijini Dar es salaam unaendelea vizuri mpaka kufikia Aprili 2018 ujenzi wa barabara ya banana kwenda Kinyerezi  hadi Kifuru ambayo ijaunganisha na barabara ya Nyerere na Morogoro umefikia asilimia 90 na imebaki kipande wa kilomita 2.