Back to top

Serikali inavitambua vyeti vyote vya kuzaliwa - MAHIGA

12 December 2019
Share

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Augustine Mahiga amesema Serikali inavitambua vyeti vyote vya kuzaliwa vinavyoendelea kutolewa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kuwa ni vyeti halali vikiwemo vile vinavyoandikwa kwa mkono kutokana na hoja zinazoendelea kutolewa na watu mbalimbali kuwa vyet i vya aina hiyo havitambuliki kwa mujibu wa sheria.

Waziri Mahiga amesema hayo Mjini Morogoro baada ya kuzindua mpango wa usajili wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Morogoro na Pwani, ambapo watoto zaidi ya Elfu kumi wamesajiliwa.