Back to top

Serikali itaendelea kudhibiti matumizi ya fedha za Umma - Majaliwa.

06 July 2020
Share

KALAMBO.

__________

Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kudhibiti matumizi ya fedha za umma, ili iweze kuendeleza ujenzi wa miradi ya kimkakati, zikiwemo bandari kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wake.

Amesema changamoto ya usafirishaji wa mizigo na abiria kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo itakuwa historia baada ya kuboreshwa na kujengwa kwa miundombinu ya bandari katika wa Ziwa Tanganyika, ukiwemo upanuzi wa bandari ya Kasanga.

Mhe.Majaliwa amesema hayo alipozungumza na wananch,i baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Bandari ya Kasanga wilayani, mradi unaotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni nne na milioni mia saba.

Amesema upanuzi wa bandari hiyo utawezesha mizigo inayotoka nchini kwenda Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kufika kwa wakati kwa sababu itasafirishwa moja kwa moja bila kupitia katika nchi nyingine kama ilivyo sasa, ambapo madereva wanalazimika kupita kwenye mataifa mengine na kutumia muda mrefu.