Serikali imesema itaendelea kuboresha sheria zinazohusiana na kuwashughulikia watu wenye tabia za kuwadhalilisha watoto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Dakta. FAUSTINE NDUGULILE amesema hayo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara hiyo.
Amesema hali hiyo inatokana na vitendo hivyo kuendelea kukithiri katika jamii na ametoa wito kwa jamii kuwafichua watu wenye tabia hizo za kuwadhalilisha watoto.
Baadhi ya wabunge waliitaka Serikali kubadilisha sheria zinazohusiana na watu ambao wanadhalilisha watoto ikiwemo kuwaasi wanaofanya vitendo hivyo.